banner here

Lazio kuzipiku klabu za England kumnasa Samatta?

- June 19, 2019
advertise here


Lazio kuzipiku klabu za England kumnasa Samatta?
 17 Juni 2019
Sambaza habari hii Email Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Whatsapp
Image copyright GETTY IMAGES
Klabu ya SS Lazio ya nchini Italia imeingia kwenye kipute cha kumnasa mshambuliaji kinara wa klabu ya Genk na timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta.

Samatta amengara sana msimu wa 2018/19 uliokwisha hivi karibuni akiiongoza safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi ya Ubelgiji baada ya miaka nane.

Kwa upande wa timu ya Tanzania, Taifa Stars chini ya unahodha wa Samatta wamefuzu kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kusubiri kwa miongo minne.

Samatta: Naweza kuvaa viatu vya Lukaku Man United
Brighton, Leicester, Roma na Lyon zamuwania Samatta
Tayari Samatta amekwisha weka wazi kuwa hatarajii kurudi Genk msimu ujao, na ana ndoto za kuhamia katika ligi ya Primia ya England.

Vilabu kadhaa vya England vikiwemo Brighton, Aston Villa, Watford, Leicester na Burnley vimehusishwa na kutaka kumsajili Samatta.

Sasa, klabu hiyo ya Lazio ambao ni miongoni mwa vilabu vikongwe na vyenye mafanikio nchini Italia inaonesha nia ya kutaka kumnyakua mshambuliaji huyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya klabu hiyo iitwayo La Lazio Siamo Noi (Sisi ni Lazio) wanamthaminisha Samatta kuwa na gharama kati ya Euro milioni 10 mpaka 12.

Tovuti hiyo inasema japo Samatta hana mwili mkubwa lakini ana kasi, akili na mzuri kwa mipira ya juu (ya kichwa); "...anaweza kuwa jina (kubwa) la kuliangalia."

Image copyright TFF/TWITTER
Lazio imemaliza katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Serie A katika msimu uliopita na haitashiriki mashindano ya bara Ulaya mwaka uliopita.

Samatta pia anaripotiwa kuzivutia klabu za AS Roma ya Italia na Lyon ya Ufaransa.

Mchezaji huyo na uongozi wake bado wapo kimya juu ya maendeleo ya harakati za usajili.

Hivi Karibuni amesema kuwa atalizungumzia suala la usajili pale muda muafaka utakapofika.

Je Samatta na Wanyama watazisaidia timu zao dhidi ya wapinzani?
Pogba: Huu ndio muda wa kuondoka Man United
Kwa nini wanawake na wanaume hawawezi kucheza mpira pamoja?
""Kwa sasa hivi siwezi kusema sana, ni kitu ambacho kipo kwenye mchakato nasubiria kitakapokuwa tayari na wakati utakapofika nitaweza kukizungumza. Lakini sijioni tena Genk, namuomba Mwenyezi Mungu litimie, lakini ikishindikana bado nina mkataba na Genk."

Streka huyo mwenye miaka 26, ameifungia Genk magoli 23 na kumaliza kama mshambuliaji bora wa ligi. Pia ameifunga magoli 9 kwenye michuano ya ligi ya Europa.

Jina la Samatta limekuwa likiimbwa na mashabiki wa Genk, na wamekuwa wakimuomba mshambuliaji huyo kusalia klabuni hapo kucheza ligi ya Mabingwa Ulaya.

Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe Januari 2016 ambapo alitia saini mkataba wa kumuweka katika klabu hiyo hadi msimu wa 2019/20.

Kabla ya kujiunga na Mazembe alikuwa akiichezea klabu ya Simba ya Tanzania.
Advertisement advertise here

 

Start typing and press Enter to search